IDARA YA KILIMO WILAYA YA MISUNGWI

Wageni kutoka idara ya kilimo ya Halimashauri ya wilaya ya misungwi wafanya ziara katika kiwanda cha Fakama Warehouse and Processing Co.Ltd kilichopo Wilayani misungwi katitka kijiji cha Mapilinga

Idara ya kilimo ya Halimashauri ya wilaya ya misungwi, imekua karibu na kampuni ya Fakama Warehouse and Processing Co.Ltd na kuwa moja ya sababu inayochangia kampuni kuendelea kufanya kilimo cha malighafi zake ili kuhakikisha inakua na malighafi ya kutosha uzalishaji kwa muda wote.


kutokana na usauri wa kitaalamu kutoka idara hiyo kampuni imeweza kuanzisha kilimo kikubwa cha Alizeti ikishirikiana na idara hiyo ili kuweza kuhakikisha kampuni inafanya kilimo cha kisasa na chenye matokeo chanya.

Picha hapo inaonyesha shamba lililopo katika sehemu ya eneo la kiwanda Mapilinga -Misungwi , ikiwa ni moja ya matokeo ya ugeni huu

Picha hapo juu ni shamba la Alizeti lenye ukubwa wa ekari 10 , lililokodiwa na kupandwa na kampuni katika kijiji cha Lubuga wilayani misungwi . pia Idara ya kilimo ya wilaya ya misungwi imekua bega kwa bega nasi hadi kufikia hatua hii.

Picha hapo juu inaonyesha shamba tulilo kodi kwa shirika la Nyanza Coperative Uninon (NCU) lenye jumla ya Ekari 100 lililo limwa na kupandwa Alizeti , pia hadi kufikia hatua hii idara ya kilimo ya Halimashauri ya wilaya ya misungwi imekua karibu kutoa ushauri juu ya kilimo hiki.